title : Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo
kiungo : Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo
Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amewasili nchini leo Jumapili, Januari 14 kwa ziara ya siku moja.
Rais Kagame aliyepokewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alielekea katika chumba maalum na kukaa kwa takribani dakika 30.
Aliondoka uwanjani hapo saa 4:47 asubuhi kuelekea Ikulu ambako atafanya mazungumzo na Rais Magufuli.
Hii ni mara ya pili kwa rais huyo kutembelea Tanzania tangu mwaka 2015, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016 ambako alishiriki maonyesho ya 40 ya kimataifa ya biashara (sabasaba).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpogea mgeni wake Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame mara baada ya kuwasili mapema leo nchini kwa ziara ya siku moja. .Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame akisalimiana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili mapema leo nchini kwa ziara ya siku moja. Pichani kulia ni Rais Dkt John Pombe Magufuli na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga .Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame aliyewasili mapema leo katika uwanja wa ndege wa Kimaifa wa Julius Nyerere (JNI),akiwa katika ziara yake ya siku moja nchini
Burudani pia ilitolewa wakati wa makokezi ya Rais wa Rwanda.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa pichani kulia akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh.Kisare Makori (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Alli Hapi wakati wa mapokezi ya Rais wa Rwanda Mh Paul Kagame aliyewasili mapema leo asubuhi nchini kwa ziara ya siku moja
Hivyo makala Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo
yaani makala yote Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/hivi-ndivyo-rais-kagame-alivyotua.html
0 Response to "Hivi Ndivyo Rais Kagame alivyotua Tanzania Hii leo"
Post a Comment