title : Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma
kiungo : Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma
Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.
"Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa" amefafanua Dkt. Abbasi.Aidha, Dkt. Abbasi ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.
“Mkiwa kama Kampuni ya Magazeti ya Serikali mnatakiwa kuibeba agenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda" ameongeza Dkt.Abbasi.
Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita katika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaeleza watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) umuhimu wa kubeba ajenda ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda wakati wa ziara yakutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma iliyoanza mapema leo.
Muwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Mkoani Dodoma Bw.Felix Mushi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika Ofisi za Kampuni hiyo Mkoani Dodoma.
Watumishi wa Gazeti la Mwananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma iliyoanza Januari 17, 2017.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Mkoani Dodoma mara baada ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo na kuzungumza na wafanyakazi, kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Gazeti la Mwananchi.(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma
yaani makala yote Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/dkt-abbas-atembelea-vyombo-vya-habari.html
0 Response to "Dkt. Abbas Atembelea Vyombo vya Habari Mkoani Dodoma"
Post a Comment