title : TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA
kiungo : TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA
TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA
Tanzania kupitia programu ya Kidunia ya Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services - GFCS) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa imefanikiwa kuandaa na kuzindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia vijana na kazi mhe. Anthony Mavunde (MB) kwa niaba ya mhe. Jenista Mhagama(MB) Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu alisema uzinduzi wa mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini utasaidia kufahamu mahitaji sahihi kwa watumiaji wa taarifa za hali ya hewa na kuongeza uhitaji wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa. Aliongeza kwa kuwataka wananchi wazitumie huduma za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania hasa ukizingatia kuwa huduma hizo zimeboreshwa na usahihi wa utabiri umeongezeka hadi kufikia zaidi ya 80%
‘Nimeelezwa kuwa Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini unatoa fursa ya kipekee katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kujenga uwezo wa watoa huduma za hali ya hewa na watumiaji, aidha ushirikiano kati ya mtoa huduma za hali ya hewa na watumiaji utaongezeka. Vilevile, mfumo huu utasaidia kufahamu mahitaji sahihi kwa mtumiaji wa taarifa za hali ya hewa ambapo utasaidia kuongeza uhitaji wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa’ alisema mhe. Mavunde.
Naibu Waziri wa Vijana na Kazi Mhe. Anthony Mavunde (MB), Katibu Mkuu (Sera na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. Petteri Taalas wakionesha mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Hivyo makala TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA
yaani makala yote TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tanzania-yazindua-mfumo-wa-taifa-wa.html
0 Response to "TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA"
Post a Comment