title : YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI
kiungo : YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI
YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI
Kikosi cha Yanga hii leo Augusti 23, 2018.

Kikosi cha Mtibwa wa Sugar leo Augusti 23, 2018.
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa akijaribu kumtoka beki wa Mtibwa wa Sugar Cassian Ponera katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa.
Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul (jezi Kijani) akipambana na mchezaji wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa.
Beki wa Mtibwa Sugar Hassan Isihaka akiwa anapambana na mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo (kushoto) katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib akiwa anamiliki mpira mbele ya kiungo wa timu ya Mtibwa Ismail Aiden katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 uliochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 12 jioni ilichukua dakika 31 kwa Timu ya Yanga kuandika goli la kuongoza kupitia kwa Mshambuliaji wake raia wa Congo Heritier Makambo akipokea pasi kutoka kwa Feisal Salum ' Fei toto'.
Dakika ya 40, beki wa Mtibwa anafanya makosa kwa kumuangusha Makambo ndani ya eneo la hatari na Yanga kupata penati iliyolipgwa na Nahodha Kelvin Yondani na kuaindikia Yanga goli la pili.
Mpaka dakika 45 ya kipindi cha kwanza kinamaliza Yanga walienda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa pande zote kushambuliana, umakini mdogo wa safu ya ushambuliaji ya Yanga kupitia kwa Makambo anakosa nafasi tatu za wazi.
Katika dakika ya 72, Mashambulizi yakiendelea langoni mwa Yanga , Mtibwa anaandika goli lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Haruna Chanongo akimalizia mpira uliopanguliwa ma goli kipa Beno Kakolanya.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga anatoka mbele kwa ushindi wa goli 2-1 unaompatia alama tatu muhimu akiwa sawa na timu zingine za ligi kuu.
Yanga ilianza mechi yake ya Ligi kuu ikiwa na wachezaji wapya Mrisho Ngasa aliyerejea msimu huu akitokea Ndanda, Deus Kaseke akiwa ametoka kuitumikia Singida United, Feisal Salum akitokea JKU ya Zanzibar pamoja na Heritier Makambo kutoka Fc Lupopo ya DR Congo.
Katika michezo mingine iliyopigwa leo Azam Fc wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa uwanja wa Azam Complex, JKT Tanzania akitoka sare 0-0 dhidi ya KMC, Stand United akiibuka na ushindiwa goli 1-0 dhidi ya African Lyon.
Hivyo makala YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI
yaani makala yote YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/yanga-yaanza-na-ushindi-wa-kwanza-wa.html
0 Response to "YANGA YAANZA NA USHINDI WA KWANZA WA LIGI"
Post a Comment