WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18

WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18
kiungo : WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18

soma pia


WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18

Na. Paschal Dotto.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwamba deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 .

Dkt. Mpango alisema kuwa katika tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

“Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonesha kuwa deni hili ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, alisema Dkt. Mpango.Akieleza takwimu hizo, Waziri Mpango amesema kuwa mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, deni la Taifa lilifikia shilingi bilioni 47,823.1 ikilinganishwa na bilioni 42,552.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2016 ambapo kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 13,417.5 ni deni la ndani sawa na asilimia 28.1 na shilingi bilioni 34,405.6 ni deni la nje ambalo ni sawa na asilimia 71.9.

Dkt. Mpango alisisitiza kuwa ongezeko hilo lilitokana na kupatikana kwa mikopo mipya ya nje na ndani ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maeneeleo.Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa mradi wa umeme Kiwira (Kiwira Coal Mine), miradi ya uboreshaji wa huduma za maji kwa jamii, mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa kinyerezi na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege ambapo miradi hiyo itawezesha watanzania kufika uchumi wa kati wenye viwanda.

“Mambo muhimu ya kujiridhisha nayo ni kwamba mikopo inayokopwa itumike katika kujenga uwezo zaidi wa kuzalisha mali na huduma nzuri kwa watanzania”, alisisitiza Dkt. Mpango.

Aidha Waziri Mpango amesema kuwa kufuatia hatua zinazochukuliwa na Serikali, ukwasi kwenye benki za biashara uliongezeka na kusaidia kupungua kwa riba ya mikopo baina ya mabenki na kufikia wastani wa asilimia 3.53 mwezi Novemba mwaka huu kutoka wastani wa asilimia 14.93 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017.Vilevile riba za dhamana za Serikali zilishuka kutoka wastani wa asilimia 15.56 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016/2017 hadi asilimia 8.76 mwezi Novemba, 2017 na kuongeza kuwa Serikali inatarajia kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi itaanza kuimarika.

Aidha, Dkt. Mpango amewaonya watu wanaotoa takwimu za uongo kuacha mara moja kwani wanaipotosha jamii, huku akiwataka waandishi wa habari kupata takwimu maalumu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuweka takwimu sahihi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maelekezo kwa Benki nchini kuangalia namna ya kupunguza riba kwa wakopaji na pia kufuata vigezo stahiki kwa mkopaji ili kuondoa mikopo chechefu wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani (kushoto) akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kulia.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)



Hivyo makala WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18

yaani makala yote WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/waziri-mpango-aelezea-hali-ya-uchumi-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MPANGO AELEZEA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/18"

Post a Comment