WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018

WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018
kiungo : WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018

soma pia


WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akifungua kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Wadau wa Elimu mkoani Simiyu wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimekuwa na mchango mkubwa katika kuuwezesha mkoani huo kushika nafasi ya kumi Kitaifa katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita  mwaka 2018, kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018 kilichofanyika Julai 24, Mjini Bariadi, ambapo pia walimu wa Kidato cha Sita waliowezesha wanafunzi kufaulu kwa alama A na B katika masomo yao wamepongezwa na kupewa zawadi ya fedha taslimu na vyeti.

Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akitoa taarifa ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018, katika kikao cha tathmini ya Matokeo hayo kilichofanyika Julai 24, Mjini Bariadi.

Kikao hiki  kimewashirikisha  viongozi na Watendaji wa Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Wakuu wa Shule na walimu wa shule za Sekondari za kidato cha tano na sita, wadhibiti ubora, Maafisa Elimu Wilaya na Kata, Wenyeviti wa Bodi za Shule, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Chama cha Walimu na wadau wengine.

Baadhi ya wadau waliochangia katika tathimini hiyo wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kuanzisha wazo la kuwa kambi za kitaaluma ambazo zimeleta mafanikio makubwa na kutoa maoni ya namna ya kuboresha na kuzifanya kambi hizi kuwa mkakati endelevu katika kuinua ubora wa elimu mkoani Simiyu.

“Nampongeza sana mkuu wetu wa Mkoa kuja na wazo hili la kuwa na kambi za Kitaaluma na Mkuu wa Mkoa amesema ni agenda ya kudumu katika mkoa , kama walimu, wazazi, wanafunzi, sisi viongozi na wadau wengine wa elimu katika Mkoa wetu tukiendelea kushirikiana, kambi hizi zitabadilisha mfumo wa elimu na kuufanya mkoa ung’are katika sekta ya elimu” Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani Simiyu, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.

“Kambi za Kitaaluma zimechangia kuufikisha mkoa kwenye nafasi ya 10 Kitaifa lakini nashauri iundwe kamati ya ndogo ya Maafisa Taaluma kutathmini mazuri na changamoto za kambi za kitaaluma ili tuweze kuboresha zaidi na kuufanya mkoa kufanya vizuri zaidi” Mwl.Baraka Owawa Katibu Chama cha Walimu Wilaya ya Bariadi.



Hivyo makala WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018

yaani makala yote WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wadau-wa-elimu-wakiri-kambi-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WADAU WA ELIMU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZACHANGIA KUIFIKISHA SIMIYU KUMI BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018"

Post a Comment