Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga

Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga
kiungo : Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga

soma pia


Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, imezindua kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa TYPF Training Centre, Saida Babde alisema ndoto yao ni Taasisi yao kuwa dira ya mtoto wa kike nchini Tanzania kwa namna moja ama nyingine, huku uzinduzi huo ukihudhuliwa na watu mbalimbali akiwamo Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Vullu na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Naseem Al Najim.

"Ndoto yetu ni kumkomboa mtoto wa kike kwa kupitia kituo chetu ambacho kitakuwa kinafundisha mambo mbalimbali kama charahani, kompyuta na kazi nyingine za mikono.

"Nawaomba Watanzania kuchangamkia fursa hii ambapo tumeanzisha ndani ya uwapo wa Taasisi yetu ya TYPF, ambapo sote kwa pamoja tuna kiu ya kumkwamua Mtanzania,"Alisema.

Naye Mheshimiwa Zainabu, Mbunge wa Viti Maalum aliwashukuru TYPF kwa kuguswa na mambo ya kijamii, hususan dhamira ya kumkwamua na kumsaidia mtoto wa kike bila kusahau wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.
 Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(wa pili kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Ally Bakry akitoa historia fupi ya uanzishwaji wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi uliofanyika kituoni hapo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre pamoja na kuomba uongozi wa taasisi hiyo kujikita zaidi kwa wasichana walioko pembezoni mwa mkoa wa Dar Es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza jambo wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Kaimu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Saida Babde akitoa ufafanuzi wa uendeshwaji wa kituo hicho na kazi zitakazofanyika kituoni hapo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DYCCC, Hassan Akrabi(kushoto) akimkabidhi cheti cha heshima kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(kulia) kwa mchango waliounesha wakati wa uanzishwaji wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem pamoja na Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri wakiwa wamekaa kwenye viti wakitumia Tarakilishi mpakato (laptop computer) wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga

yaani makala yote Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/taasisi-ya-typf-yazindua-kituo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Taasisi ya TYPF yazindua kituo cha ufundi Upanga"

Post a Comment