MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI

MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI
kiungo : MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI

soma pia


MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI

Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imetoa kipindi cha mwezi mmoja kwa mashirika na taasisi za umma zisizokamilika taratibu za kuwekeana saini ya mikataba ya utendaji kazi kwa mwaka 2018/19 kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Akizungumza katika halfla ya utiliaji saini wa mikataba ya utendaji kazi kwa Taasisi na Mashrika ya Umma 80 kwa mwaka 2018/19 leo Jumanne (Oktoba 2, 2018) Jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina Athuman Mbuttuka alisema mikataba hiyo ya kazi ni utekelezaji wa sharia na Serikali itaendelea kusimamia  Taasisi na Mashirika yao ili yaweze kufikia malengo yaliyowekwa.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwekana saini na taasisi na mashirika ya umma 105 na kutaka taasisi zingine zilizobaki kukamilisha taratibu hizp kabla ya Serikali haijaanza kuzichulia hatua kwa mujibu wa Sheria.
Akifafanua zaidi alisema Ofisi yake imesajili jumla ya Taasisi na Mashirika ya Umma 185 kati ya makampuni, mashirika, wakala na taasisi 233 zilizopo nchini ambazo  baadhi yake zimeunganishwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa umma.
Mbuttuka alisema mikataba hiyo imelenga katika kuhakikisha kuwa Serikali na mashirika yanawekeana na ili kuwa na na mwelekeo unaowiana katika kuongeza ufanisi katika maeneo makuu manne ikiwemo Utawala Bora, rasilimali fedha, mikataba ya huduma kwa wateja na uzingatiaji wa kanuni, sharia na taratibu.
 “Tumewekeana mikataba na Wenyeviti wa Bodi katika mashirika na taasisi za Umma katika kuhakikisha kuwa yanaongeza tija na ufanisi katika kuleta matokeo chanya katika maeneo ya kazi pia kuwaweka kwa karibu zaidi Menejimenti na Bodi kufahamu wajibu na majukumu yao katika taasisi hizo” alisema Mbutuka.
Aidha alisema katika mikataba hiyo, Serikali iliweka mkazo katika maeneo hayo manne kwa kutambua kuwa ni sehemu muhimu zilizohitajika kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha utoaji huduma na kufanya mashirika na taasisi za umma kuweza kujiendesha vyema na kuleta tija kwa Serikali na Umma kwa ujumla.
“Katika hili eneo la rasilimali watu tumeangalia ni mafunzo, muundo na motisha kwa watumishi zinawezesha watumishi kutekeleza vyema majukumu yao lakini pia eneo la usimamizi wa fedha tumeangalia ni kwa namna gani tutaweza kupunguza gharama zisizo za lazima katika taasisi na mashirika haya” alisema Mbuttuka.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi akisaini Mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/2019 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi hiyo na Serikali wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba baina ya Taasisi na na Serikali Mashirika ya Umma  zoezi leo  jumanne Oktaba 2,2018. Kulia ni Kamshina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijan Mssanzya.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL), Mhandisi Omary Nundu akisaini Mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/2019 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi hiyo na Serikali wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba baina ya Taasisi na na Serikali Mashirika ya Umma  zoezi leo  jumanne Oktaba 2,2018.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda akikadhi nakala ya mkataba wa utendaji kazi kwa mwaka 2018/19 mbele ya Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka kati ya Taasisi na Mashirika ya Umma wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba baina ya Taasisi hizo  na Serikali iliyofanyika leo jumanne Oktoba 2, 2018. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Rosebud Kurwijila wakati wa hafla utiaji saini baina ya Taasisi na Mashirika ya Umma na Serikali kwa mwaka 2018 iliyofanyika leo Jumanne Oktoba 2, 2018.
 Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka (katikati) akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema  wa wakati ya saini baina hafla ya utiaji Taasisi na Mashirika ya Umma na Serikali kwa mwaka 2018/2019, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, hafla iliyofanyika  leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI

yaani makala yote MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mashirika-ya-umma-yapewa-mwezi-mmoja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASHIRIKA YA UMMA YAPEWA MWEZI MMOJA KUSAINI MIKATABA YA UTENDAJI KAZI"

Post a Comment