title : SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile
kiungo : SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile
SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO ZIKISISITIZA JUU YA WAJIBU WA WATOA HUDUMA ZA AFYA NA MABARAZA YA KITAALUMA PAMOJA NA HAKI ZA WANANCHI KUPATA HUDUMA BORA ZA AFYA.
Ndugu Wananchi,
Nachukua fursa hii kuungana nanyi nyote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha salama siku hii ya leo tunapoanza mwaka mpya 2018. Hii ni neema pekee ambayo Mwenyezi Mungu ametujaalia kwani kuna wengi walitamani kuifikia siku hii lakini hawakubahatika. Hivyo, nawatakieni nyote kheri na fanaka katika mwaka huu mpya.
Napenda kutumia fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza Wanataaluma na Watoa huduma za afya wote kwa kuendelea kutoa huduma kwa ari, juhudi, uaminifu na uadilifu licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. Nami nawatia shime na hamasa ili muendelee na moyo huo wa kuwahudumia na kuwatumikia Wananchi.
Natambua kuwa Sera yetu ya Afya inataka tuijenge jamii yenye afya bora na ustawi ambayo itachangia kikamilifu katika maendeleo ya mtu binafsi pamoja na yale ya Taifa. Aidha, Sera na Sheria zetu mbali mbali zinatambua umuhimu na nafasi ya Mabaraza ya kitaaluma katika kuboresha na kusimamia viwango vya maadili ya wanataaluma walio chini ya Wizara yangu. Jambo hili ni muhimu sana hususan tukizingatia ongezeko la minong’ono, manung’uniko na hata malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya baadhi ya watoa huduma ambao wanakiuka taratibu au miiko ya kazi zao na hivyo kuathiri ubora wa utoaji huduma.
Nimeona kama sehemu ya salamu zangu za mwaka mpya wa 2018, nitoe maelekezo yatakayoweza kutusaidia kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya kupitia Watoa Huduma za Afya na Mabaraza ya Kitaaluma na pia kuwakumbusha wananchi juu ya haki yao ya msingi ya kupata huduma bora za afya na wajibu wao wa kuhakikisha hilo linatokea.
Hivyo makala SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile
yaani makala yote SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/salamu-za-mwaka-mpya-kutoka-kwa-mhe.html
0 Response to "SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MHE. NAIBU WAZIRI WA AFYA Dkt. Faustine Ndugulile"
Post a Comment