Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara

Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara
kiungo : Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara

soma pia


Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara

“Jioni hii nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mkuu wa Mkoa Mstaafu Dkt. Joel Nkaya Bendera, natoa pole kwa familia yake na wote walioguswa na msiba huu na pia naungana nao katika kipindi hiki cha majonzi”

Hii ni sehemu ya salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizozitoa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Nkaya Bendera kilichotokea jioni ya leo tarehe 06 Desemba, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikofikishwa kwa ajili ya kupata matibabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Dkt. Joel Bendera atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa akiwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Naibu Waziri na Mbunge na pia kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo.

“Dkt. Joel Nkaya Bendera alikuwa kiongozi shupavu, mahiri na mchapakazi, alipenda kufanya kazi kwa ushirikiano na daima alitamani kupata mafanikio makubwa katika majukumu aliyokuwa nayo, hakika tutamkumbuka” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Pamoja na kutoa pole kwa familia ya marehemu, Mhe. Rais Magufuli amewapa pole wananchi wa Mkoa wa Manyara ambako alikuwa Mkuu wa Mkoa hadi tarehe 26 Oktoba, 2017, wananchi wa Mkoa wa Tanga ambako alikuwa Mbunge, wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wanamichezo wote na wote walioguswa na msiba huu na amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2017


Hivyo makala Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara

yaani makala yote Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/rais-magufuli-aomboleza-kifo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Magufuli aomboleza kifo cha aliyekuwa RC Manyara"

Post a Comment