title : KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO.
kiungo : KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO.
KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO.
Kampuni ya Star Media (T) Ltd imefikia makubaliano na shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) katika utoaji wa elimu na matangazo kupitia kampuni hiyo ili kuhakikisha ifikapo 2030 gonjwa la UKIMWI linatokomezwa .
Makubaliano hayo baina ya Kampuni ya Star Media (T) Ltd na UNAIDS yametiliwa saini leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za Ubalozi wa China na kuhudhuriwa na Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong, wawakilishi wa UNAIDS, Mkurugenzi wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Startimes na UNAIDS zimefikia makubaliano ya pamoja ili kuhakikisha wanafikia lengo la kutokomeza UKIMWI katika ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Star Media (T) Ltd, Wang Xiaobo amesema Startimes na UNAIDS zitashirikiana pamoja katika kutoa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ukimwi ili kupunguza unyanyapaa na kutengwa miongoni mwa waathirika wa virusi vya ugonjwa huo, katika maeneo mbalimbali ambayo kampuni ya startimes tayari inarusha matangazo yake.
" Tutahamasisha kupima, kulinda na kumaliza unyanyapaa, ugonjwa wa Ukimwi ni adui mkubwa kote duniani na sisi kama startimes tunajisikia fahari kuungana na UNAIDS katika mapambano haya” amesema Wang.
Mkurugenzi wa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) nchini Tanzania, Dkt.Leopold Zekeng(kulia) wakitiliana sahihi ya makubaliano ili kuhakikisha wanafikia lengo la kutokomeza UKIMWI katika ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2030. Katikati ni Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong.
Mkurugenzi wa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo pamoja na Mkurugenzi akipeana mkono na Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) nchini Tanzania, Dkt.Leopold Zekeng(kushoto) mara baada ya kumaliza kutiliana sahihi. Katikati ni Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong.
Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong(katikati) akizungumza na wadau wa Ukikwi pamoja na waandishi wa habari kuhusu kuhusu mchango wa China katika kupambana na gonjwa la Ukimwi nchini Tanzania.
Hivyo makala KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO.
yaani makala yote KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/kampuni-ya-star-media-t-ltd-yaingia.html
0 Response to "KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO."
Post a Comment