title : MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA
kiungo : MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA
MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameigizaa Bodi ya Barabara kuhakikisha fedha za mkopo ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara zinatumika ipasavyo
Amesema fedha hizo zinatakiwa kujenga barabara za kisasa na si kutumika kwenye warsha, semina na safari za mafunzo nje ya nchi.
Akizungumza leo, Makonda amesema Dar es salaam ina fedha za DMDP takribani Sh.bilioni 600 kwa ya kujenga barabara na mifereji lakini asilimia kubwa ya fedha hizo zimekuwa zikitumika kwenye semina na safari za nje ya nchi kujifunza namna ya usimamizi wa barabara.
"Jambo jambo linalosaabisha Serikali kulipa madeni kwa mirado ambavyo imekusudiwa," amesema Makonda.
Pia Makonda amegundua gharama ya kujenga barabara ya Kilometa moja kwa fedha ya DMDP ni sawa na gharama ya kujenga barabara ya TANROAD Kilometa 3, hivyo ameshauri kikao hicho kuangalia kwa umakini jambo hilo ili fedha hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi kwa uwepo wa barabara zenye ubora.
Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2018-2019 Mkoa wa Dar es salaam umetenga Sh.bilioni 289.3 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini(TARURA),Tanroad na vyanzo Wakala wa Barabara za Mjini na vya ndani vya halmashauri.
Ameongeza hataki kuona w,ananchi wa Dar es Salaam wanateseka kutokana na ubovu wa barabara zenye mashimo na mahandaki.
Amesema hali hiyo husababisha hasara ya uharibifu wa vyombo vya usafiri na wakati mwingine ongezeko la msongamano wa magari.
"Nimeanza kuona nuru baada wakandarasi wa barabara za Dar es salaam kuanza kufuata taratibu kwa kutengeneza barabara za kisasa.Niwasihi TARURA m uwe wasimamizi wazuri wa ujenzi barabara kama wanavyofanya TANROAD ili tuwe na barabara zinazodumu muda mrefu," amesema Makonda.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo jijini.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(kushoto) pamoja na wajumbe wakingine wakiwa kwenye kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar
Hivyo makala MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA
yaani makala yote MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/makonda-ataka-fedha-za-mkopo-wa.html
0 Response to "MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA"
Post a Comment