JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018
kiungo : JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

soma pia


JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

Angela Msimbira – OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 Tanzania Bara kwenye kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Jafo amesema kuwa idadi wa wanafunzi mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2016.

Amesema kuwa wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za Serikali.

Mhe. Jafo amefafanua kuwa wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya Halmashauri ya Mikoa ya Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo kwenye mkutano i kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akifafanua jambo wakati akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.




Hivyo makala JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

yaani makala yote JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/jafo-atangaza-waliochaguliwa-kujiunga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAFO ATANGAZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018"

Post a Comment