title : MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)
kiungo : MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)
MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)
Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii
Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) limeipa wenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika taifa la Misri kwa mwaka huu wa 2019 baada yakuishinda Afrika Kusini kwa kura zakuwania uandaaji wa Michuano hiyo.
Mashindano hayo yalikuwa yaandaliwe na taifa la Cameroon kwa mwaka huu, mwezi Novemba CAF iliipokonya maandalizi hayo kutokana na kuwa na maandalizi hafifu. Misri itakuwa na muda wa miezi 6 tu kufanya maandalizi kwa ajili ya ugeni wa Mataifa 24 yatakayoshiriki Michuano hiyo mwezi June.
Hata hivyo itakuwa ni mara ya Tano kwa Misri kuandaa Mashindano hayo tangu mara ya mwisho mwaka 2006 ilipoandaa Mashindano hayo."Napenda kuishukuru Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF) kwa kutuamini kuandaa Mashindano haya makubwa barani Afrika na naishukuru Serikali yetu kwa kuunga mkono suala hili,’ amesema Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Misri (EFA), Hany Abu Rida.
"Tuliandaa Mashindano haya 2006 ambapo ilitupa sana changamoto kufanya vizuri, lakini kwa sasa tuko vizuri,’ amesema Abu Rida."Serkali imetuhakikishia kutusaidia ili kuhakikisha tunashuinda dhidi ya Afrika Kusini ambapo pia itatusaidia kufanya vizuri katika mashindano haya, Mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi viwanjani naamini tutakuwa vizuri katika mashindano haya, amesema Makamu wa Rais wa EFA, Ahmed Shobair.
Misri itatumia viwanja Nane katika Mashindano hayo, vitakavyokuwa katika Miji Mitano ya Alexandria, Ismailia, Port Said, Suez na Mji Mkuu wa Cairo.CAF inatarajia kuitangaza rasmi Misri Jumatano ya Januari 9 kuwa ni mwenyeji wa Mashindano hayo.
CHANZO: BBC SPORTS
Hivyo makala MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)
yaani makala yote MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/misri-yapewa-wenyeji-wa-michuano-ya.html
0 Response to "MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)"
Post a Comment