title : Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza
kiungo : Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza
Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza
Na George Binagi.
Wananchi jijini Mwanza wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye “Kongamano la Watoa Tiba kwa Vitendo”, litakalofanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Kanda Bugando jijini Mwanza kuanzia jumatano Novemba 29 hadi ijumaa Disemba Mosi mwaka huu, ili kupata huduma ya ushauri kuhusiana na matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa.
Hata hivyo huduma hiyo itatolewa kwa wananchi siku moja tu ambayo ni jumatano Novemba 29, ambapo watahudumiwa bure kuanzia majira ya asubuhi.
Akizungumza na BMG, Mratibu wa kongamano hilo Dr.Joyce Karawa amesema wananchi watapata huduma ya ushauri nasaha bure kuhusiana na mitindo ya kimaisha inayopelekee ulemavu wa kimwili na kiakili na pia namna ya kujiepusha.
“Tunatarajia kuwa na wataalaumu wa afya kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali ya Rufaa KCMC, hospitali ya magonjwa ya akili Mirembe pamoja na nyinginezo hivyo tunawasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hiyo bure”. Amesema Dr.Karawa.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania (Tanzanian Occupational Therapists Association-TOTA), likiwa na kauli mbiu ihimizayo “Kutanua Wigo wa Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Kujenga Uhuru wa Kujitegemea” ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Hivyo makala Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza
yaani makala yote Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/wananchi-kuhudumiwa-bure-bugando-jijini.html
0 Response to "Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza"
Post a Comment