title : RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA
kiungo : RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA
RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA
Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kwa uadilifu wakitambua kuwa sasa Mkoa wa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Aidha amesema yapo baadhi ya maeneo Mkoa bado haufanyi vizuri hususani katika sekta ya elimu ambapo hali ya ufaulu hairidhishi.
Akiwa wilayani Mpwapwa katika ziara yake ya kutembelea wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Dkt. Mahenge amesema eneo la Elimu ya Msingi na Sekondari hali ya ufaulu hairidhishi ambapo Mkoa umeshika nafasi ya 24 kati ya Mikoa 26 kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017, Wakati kwa upande wa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne mwaka 2016 Mkoa ulikuwa wa 19 kati ya Mikoa 26.
Amesema viongozi hao wanayodhamana kubwa kwa Wanadodoma kwenye masuala yote ya maendeleo kama vile Elimu, Afya, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kutumia fursa ya kuwa jirani na Serikali katika kusukuma mbele masuala ya Maendeleo kwenye Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akikagua kitalu cha miche ya Mikorosho ambayo itaanza kugaiwa bure kwa wananchi kwa lengo la kuipanda na kukuza kilimo cha zao la korosho wilayani Mpwapwa
Sehemu ya Kitalu cha Miche ya Mikorosho kilichopo eneo la Magereza Mpwapwa, jumla ya tani sita (6) za mbegu bora za mikorosho zimeoteshwa kwa lengo la kugawa bure miche ya mikorosho kwa wananchi kuipanda na kukuza kilimo cha zao hilo Wilayani Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge namna miti ya mikorosho ilivyozaa korosho kwenye shamba darasa la Magereza Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kukamua mbegu za alizeti na usindikaji mafuta ya alizeti cha mjasiriamali Ndg. Sangito Akyoo.
Hivyo makala RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA
yaani makala yote RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rc-mahenge-atoa-neno-kwa-watumishi.html
0 Response to "RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA"
Post a Comment