ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI
kiungo : ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

soma pia


ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Imma Msumba

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro anakusudia kupeleka Ombi Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kufuta Hati za baadhi ya Mashamba makubwa ya ardhi ambayo wamiliki wake wamebainika kuwa chanzo cha kuvuruga Amani na Usalama Kutokana na kuwepo Kwa migogoro ya muda mrefu ambayo baadhi imegharimu maisha ya wananchi pamoja na uharibifu wa Mali.

Dc Muro Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili uku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .

Mhe. Muro ambae alilazimika kutembea Kwa miguu katika Kata nzima ameshangazwa kuona wananchi wengi wenye Uwezo wa kulima wakishindwa kulima Kutokana na baadhi ya wawekezaji na wamiliki wa maeneo hayo kushindwa kuyaendeleza hatua iliyosababisha wananchi kuamua kuvamia Mashamba hayo na kulima kienyeji hatua ambayo imeibua Migogoro mikubwa ya ardhi, ambapo amesisitiza Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Wawekezaji wanawekeza Kwa nia ya dhati na sio kuhodhi Mashamba makubwa ambayo wameshindwa kuyaendeleza na hatimae kutoa mwanya Kwa wananchi kuvamia na kisha kuibua migogoro.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua maeneo hayo katika viwanja vya chama cha Ushirika Sing’isi Mhe. Muro amesema katika hatua za awali ametumia Busara ya kumtaka Ndugu Aloyce Kimaro mmiliki wa Hotel ya Nakara kutokanyaga Eneo la Madira Sing’isi alilokuwa akitaka kubadilisha matumizi ya Ardhi, hatua iliyosababisha Kuibuka Kwa vurugu kubw,Vifo pamoja na uharibifu wa Mali katika Eneo hilo.

Hapo awali Ndugu Kimaro alipewa Eneo hilo na Wizara ya Kilimo Kwa ajili ya uwekezaji wa hotel Kubwa Kwa ajili ya Mkutano wa kimataifa,ambapo taarifa zinaonesha kuwepo na viashiria vya uvunjifu wa Amani endapo Ndugu Kimaro atarejea katika Eneo hilo kwani taarifa za awali zinaonyesha kuwepo Kwa utata wa njia alizotumia kumilikishwa Shamba hilo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama kuendelea kulichunguza jambo hilo Kwa umakini mkubwa
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mh.Jerry muro akihutubia wananchi wa Kata ya singisi
 Dc Muro akiwa na ujumbe wake akiwa katika ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili huku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akifafanuliwa jambo na  Afisa Mtendaji kata wa Singisi.

 


Hivyo makala ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

yaani makala yote ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/arumeru-waazimia-kumaliza-migogoro-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI"

Post a Comment