NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43.

NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43.
kiungo : NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43.

soma pia


NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43.


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa maandalizi ya vifaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaofanyika katika kata 43 yamekamilika na awamu ya pili ya vifaa vitaanza kusafirishwa leo Ijumaa kwenda katika kata husika.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Kailima Ramadhani, alisema kwamba vifaa vitakavyosafirishwa kuanzia kesho ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, makarani waongozaji pamoja na  mfano wa karatasi za kupigia kura.
 
Alisema awamu ya kwanza ya kusafirisha vifaa ulifanywa na tume wakati wa mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ambayo yalifanyika mjini Dodoma ambavyo vilitumika wakati wa uteuizi wa wagombea udiwani katika kata zote.
 
“Napenda kuwahakikishia umma kwamba tume imejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu na maandalizi ya kupeleka vifaa katika husika yako vizuri na awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa itapaelekwa kesho (leo),”alisema Ramadhani.
 
Alisema awamu ya tatu ya usafirishaji wa vifaa itahusisha  vifaa vichache ambavyo ni karatasi za kupigia kura pamoja na fomu za kutangazia washindi ngazi ya kituo na ngazi ya kata.
 
Naye Mkurugenzi wa Manunuzi, Ugavi na Logistiki wa NEC Eliud Njaila, alisema kwamba NEC imepeleka vifaa vya kutosha katika vituo vyote 893  vilivyoko katika kata 43 na hakutakuwa na upungufu wowote.
 
Alisema kwamba katika awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa, wameweka na mfano wa karatasi za kupigia kura ili wadau ambavyo ni vyama vya siasa vijiridhishe kuhusu karatasi hivyo zitakavyokuwa pamoja na kufanya uhakiki wa majina wa wagombea wao.
 
“Tunaamini kwamba vyama vya siasa vitahakiki majina ya wagombea wao kwa kila kata ili kama kuna masahihisho wayalete mapema na NEC iweze kufanya masahihisho haraka wakati wa kuchapa karatasi halisi za kupigia kura,” alisema Njaila.
 
Njaila pia aliwataka wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya kuwatumia maafisa boharia katika kupokea na kutunza vifaa hivyo. Alisema wataalamu hao pia ndio watumike pia kusafirisha vifaa hivyo kwa kuwa wao wana ujuzi wa namna ya kutunza na kugawa vifaa.
 
Aliongeza kuwa iwapo wasimamizi wa uchaguzi watawatumia maafisa ugavi ni wazi kuwa hakutakuwa na malalamiko ya kupungua kwa vifaa katika vituo vya kupigia kura.
 
 Naye Ofisa Uchaguzi wa NEC Sada Kangeta, alisema kuwa tayari wameshafanya uhakiki wa vifaa vya uchaguzi na wamejiridhisha kuwa vifaa vyote vipo kama inavyopaswa na kwamba hatua itakayofuata ni usafirishaji wa vifaa hivyo katika maeneo husika.
 
Aidha aliwataka wapiga kura wote wa maeneo husika, wagombea wa vyama vyote vya siasa na wadau wa siasa kutokuwa na hofu juu ya vifaa hivyo kwa madai kuwa hakuna upungufu wowote utakaojitokeza.
 


Hivyo makala NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43.

yaani makala yote NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/nec-yasambaza-vifaa-vya-uchaguzi-mdogo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NEC Yasambaza Vifaa Vya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata 43."

Post a Comment