title : WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO.
kiungo : WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO.
WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO.
Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Rweyemamu (50) kwa mara nyingine tena, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasaidie kupata mishahara yao ili waweze kusaidia familia zao.
Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko ametoa ombi hilo leo Novemba 9/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.Nkoko aliomba mahakama isaidie familia za washtakiwa hao kupata mishahara hiyo kwa sababu wana watoto ambao wanaugua na wanahitaji huduma.
Aidha amedai wangependa kuona washtakiwa wanapata dhamana lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewawekea zuio. "Mheshimkwa tuunaomba Wateja wetu wapatiwe mishahara yao hata kwa kupitia dirishani halafu wao waendelee kushikilia hizo akaunti," alidai Nehemia.
nehemia amedai hayo baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kudai jalada la polisi la kesi hiyo lipo kwa DPP na kwamba tarehe ijayo wataeleza kwa ufasaha upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi.
Wakiendelea kuwasilisha madai yao, mawakili hao utetezi aliomba familia za washtaki zipatiwe mishahara hiyo kwa sababu chanzo chake kinajulikana kinatoka wapi na kwamba familia hizo zinahaki ya kupata mahitaji na kuwazia ni sawa ba kuwahukumu.
"Washtakiwa kabla ya kufikishwa mahakamani walikaa polisi kwa wiki tatu wakisema wanachunguza wakikamilisha upelelezi wangewalete mahakamani na tumaini letu tulidhani baada ya kuletwa mahakamani upelelezi umeishakamilika lakini wanashangaa hadi leo wanaambiwa upelelezi bado" alidai Nkoko.
Kufuatia hali hiyo, wameomba upande wa Mashtaka kueleza ni sehemu upelelezi bado haujakamilika sababu wanaamini hadi washtakiwa wanafikishwa mahakamani hapo basi upelelezi ulikuwa umekamilika.
Akijibu hoja hizo, Wankyo alimshauri Nkoko kuandika barua kwa DPP ili aweze kushughulikia suala hilo la mishahara.
Kufuatia hija hizo, hakimu Mwijage aliamuru pande zote mbili, ule Wa mashtaka na utetezi kushirikiana kulishughulikia sualala hilo ili familia hizo zipate mishahara hiyo .Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba ,23,2017.
Washtakiwa wote, Kalugendo na Rweyemamu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.
Hivyo makala WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO.
yaani makala yote WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/watuhumiwa-kesi-ya-madini-ya-almas.html
0 Response to "WATUHUMIWA KESI YA MADINI YA ALMAS WAIOMBA MAHAKAMA IWASAIDIE KUPATA MISHAHARA YAO ILI KUSAIDIA FAMILIA ZAO."
Post a Comment