BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU
kiungo : BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

soma pia


BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

Tarehe 20 Mei, 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais iliutaarifu umma kuhusu utaratibu wa kufanya shughuli zote zinazohusu ukusanyaji, usafirishaji, biashara na urejeleshaji wa taka hatarishi kama vile vyuma chakavu, "Oil" chafu, matairi yaliyotumika, taka za kieletroniki na za umeme na taka zitokanazo na kemikali. 

Ofisi iliwataka wale wote wanaofanya shughuli hizi hapa nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo. Aidha, kuzingatia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira ambayo Tanzania ni mwanachama ikiwa ni pamoja na kuwa na vibali vya biashara husika.

Ofisi inapenda kuukumbusha umma kuwa bado baadhi ya wanaokusanya, kusafirisha na kurejeleza taka hatarishi hawana vibali kama inavyohitajika. Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, kanuni ya 39 hadi 46 zinatoa muongozo wa hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa ili shughuli husika zifanyike.

Hivyo, Ofisi inawakumbusha tena wale wote wanaofanya shughuli za uuzaji na ununuzi wa taka hizi kuhakikisha wanafanya biashara na wale wenye vibali tu. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009. 

Aidha, Kanuni ya 47 (3) ya Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 inatoa adhabu kwa mtu ambaye anashindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa, ambapo baada ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000.00) au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja. 

Mhandisi Joseph Kizito Malongo

KATIBU MKUU
OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Hivyo makala BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

yaani makala yote BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/biashara-ya-chuma-chakavu-na-taka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU"

Post a Comment