title : WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN
kiungo : WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN
WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN
Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa keleza matatizo yao.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima".
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima”
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN
yaani makala yote WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/waziri-ummy-atoa-miezi-sita-kuanzishwa.html
0 Response to "WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN"
Post a Comment