title : MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI
kiungo : MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI
MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI
Efm redio inatarajia kuzima kiki zote kwa kuwasha muziki wilaya ya Kigamboni, siku ya Jumamosi ya tarehe 9/9/2017 katika Bar ya G5 ikiwa ni muendelezo wa tamasha la Mziki Mnene lililoanza wiki mbili zilizopita ambapo burudani ya muziki kutoka kwa RDJs wa EFM na wasanii mbalimbali akiwemo Sholo Mwamba, Yuda msaliti, Daina Nyange, Timbulo na wengine wengi watakiamsha katika Bar hiyo.
Na katika kuipa kipaumbele michezo, na kuinua vipaji vya vijana katika uimbaji, Efm itatafuta vipaji vya muziki wa Singeli “Singeli Michano” katika Kiwanja cha Machava ambapo mshindi katika kila wilaya atapata fursa ya kurekodi nyimbo bure, Ikifuatiwa na mechi ya kirafiki kuanzia saa 10:00 Jioni baina ya timu ya EFM na KOC Veterans katika uwanja wa Kibugumo –Kigamboni na Asubuhi Efm jogging itajumuika na jogging club za Kigamboni kukata wese na kuweka mwili fresh kwa mbio za mwendo pole.
Vilevile wakazi wa Kigamboni watapata nafasi ya kujumuika, kujadili mambo kadha wa kadha na watangazaji mahiri wa kipindi cha Joto la Asubuhi, Sports Headquarters, Uhondo, na Ladha 3600 katika kiwanja cha MACHAVA siku ya Ijumaa tarehe 8/9/2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 9:00 Alasiri ambapo vipindi hivyo vitarushwa live kutoka uwanjani hapo.
Efm mziki mnene, zima kiki washa muziki.
Hivyo makala MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI
yaani makala yote MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/mziki-mnene-wa-efm-kuzima-kiki-kigamboni.html
0 Response to "MZIKI MNENE WA EFM KUZIMA KIKI KIGAMBONI"
Post a Comment