UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP

UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP
kiungo : UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP

soma pia


UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP

 UPANDE wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuite Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP) aje kueleza kwanini jalada la kesi hiyo limekaa  ofisini kwake kwa siku 37.

Maombi hayo yamewasilishwa na Wakili Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard  Swai kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada kusikia hayo, wakili Rweyongeza amedai upande wa Mashtaka awali uliomba wiki mbili ili walete taarifa kamili kuhusu jalada hilo kutoka kwa DPP.ambapo Swai alidai hawajapata taarifa ya DPP kuhusu jalada hilo na kwamba bado wanafuatilia.

Amedai kuwa wanawasiwasi mkubwa kuwa, huenda ofisi ya DPP imeamua kuwapeleka washtakiwa gerezani na kuwaegesha kama magari kwa sababu kesi yao haina dhamana ili ikiwapendeza ndio wawachukulie hatua.
“Tunasita kusema ni matumizi mabaya ya sheria ama ni matumizi mabaya ya mamlaka ya DPP lakini hakuna lugha nzuri zaidi inabidi tuseme hivyo”, alisema Rweyongeza.

Wakili Rweyongeza aliomba mahakama imuite DPP mahakamani hapo ili afike kueleza ni nini kinasababisha upepelezi kuchelewa na ili haki ionekane inatendeka kwa muda muafaka anajukumu la kisheria la kuzingatia Haki na kutenda kazi yake kwa kuzingatia Haki. 

Wakili wa utetezi, Abrahamu Senguji alidai naye alishawahi kufuatilia jalada hilo kwa DPP bila mafanikio hivyo ni bora DPP mwenyewe aitwe mahakama kueleza ni kwanini jalada hilo limekaa ofisini kwake kwa muda mrefu au ikiwezekana upande wa mashtaka wawabadilishie washtakiwa mashtaka wapate dhamana wao waendelee na upelelezi.

Swai alisema, jalada hilo lilipelekwa kwa ajili ya kupitiwa ili atoe kibali liendelee ama upelelezi zaidi ufanyike ama hakuna ushahidi wa kutosha ifutwe.

Kufuatia mabishano marefu, Hakimu Mashauri amesema atatoa uamuzi wa hoja hizo Novemba 10,mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28, yakiwamo ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani, 375,418.


Hivyo makala UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP

yaani makala yote UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/upande-wautetezi-wa-kesi-ya-malinzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP"

Post a Comment