TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
kiungo : TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

soma pia


TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Mwambawahabari

Picha no. 1
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akizindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI Prof. William Mahalu na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Picha no. 2
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Restituta Rugaganya mara baada ya kuzindua baraza hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Picha no. 3
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rajabu Matiku  mara baada ya kuzindua baraza hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Picha no. 4
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimpongeza  Katibu wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Samweli Rweyemamu mara baada ya kumkabidhi vitendea kazi wakati wa uzinduzi wa  baraza hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha no. 5
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa baraza uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu mwenyekiti wa TUGHE Rajabu Hamisi.
picha no.8
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Ulemavu Andrew Mwalwisi wakati wa uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
picha no.9
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
picha no.10
Mkutano wa kuzindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ukiendelea.
Picha na JKCI
…………..
WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE WATAKIWA KULITUMIA BARAZA HILO KUFIKISHA MALALAMIKO YAO NA KUTOA MAONI NA SIYO VINGINEVYO
Na Mwandishi wetu
11/10/2017 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kulitumia Baraza la wafanyakazi kufikisha malalamiko yao na kutoa maoni ya utendaji kazi na siyo vinginevyo.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu  Andrew Mwalwisi wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la JKCI.
Alisema  baraza hilo ni la  muhimu kwani ndilo linalotambulika kwa mujibu wa kisheria kama watalitumia  vema kufikisha malalamiko yao,  maoni na ushauri wa sheria na si kulitumia kama ‘forum’ (majukwaa) ambayo hayatambuliki kisheria litawasaidia kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na wafanyakazi.
“Ninaimani  kubwa kwa uongozi wa taasisi hii kwamba utapokea malalamiko, ushauri na maoni ya wafanyakazi wake kupitia baraza hili na kuyafanyia kazi. Hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi hii katika kuhudumia wagonjwa (wateja)”, Mwalwisi alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema kuzinduliwa kwa baraza hilo kunadhihirisha jinsi ambavyo taasisi hiyo imekua katika utoaji huduma.
“Kwa hiyo leo kwetu ni siku muhimu kwani baraza hili lililozinduliwa ni la muhimu litatusaidia katika kuimarisha utendaji kazi wa taasisi,” alisema.
Prof. Janabi aliwasisitiza wajumbe waliochaguliwa kuliongoza baraza hilo kuwa chachu katika kutimiza wajibu wao kuisaidia taasisi kuendelea kutimiza dhima yake ya kutoa huduma bora za kimatibabu na za kitafiti ili iweze kufikia lengo iliyojiwekea la kuwa kituo bora cha kutoa huduma za afya ya moyo Afrika.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi hiyo Prof. William Mahalu aliupogeza uongozi wa Taasisi kwa kusimamia na kuhakikisha Baraza la wafanyakazi linaundwa na kuanza kufanya kazi zake kwa wakati.
Prof. Mahalu alisema tangu  kuanzishwa kwa Taasisi hiyo huu ni mwaka mmoja na nusu wameweza  kuwa na baraza la wafanyakazi jambo ambalo siyo rahisi kwani wengine wanakaa hadi miaka mitatu  wakibisahana nani awe Katibu wa kuliongoza baraza lao.


Hivyo makala TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

yaani makala yote TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/taasisi-ya-moyo-jakaya-kikwete-jkci.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI"

Post a Comment