Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya

Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya
kiungo : Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya

soma pia


Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Raia kumi wa Iran na watanzania wawili, leo Oktoba 30, 2017 wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mshtaka matatu ya kukutwa na mchanganyiko wa dawa za kulevya za Heroin Bangi na Kuberi zenye uzito wa zaidi ya kilogram 110.

Hati ya Mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi imewataja raia hao wa Iran kuwa ni, Nabibakshsh Bibarde ,40, Mohammadhanif Dorzade, 23, Abdallah Sahib,21, Ubeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Golmohamad, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Abdulmajid Asqan na Tahir Mubarak.

Pia watanzania hao ni, Ally Abdallah Ally na Juma Amour Juma.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa imedaiwa kuwa, Oktoba 25 mwaka huu, huko katika Ukanda wa Bahari ya Hindi, upande wa Tanzania washtakiwa walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 111.02 aina ya Heroine.

Aidha, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha  gramu 235.78 za Bangi.

Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha mchanganyiko wa dawa za kulevya aina ya Bangi na Kuberi zenye uzito wa kilo 3.34.

Hata hivyo, washtakiwa hao ambao walikuwa wakitafsiriwa kwa lugha ya Kiiran kutoka lugha ya kiswahili na mkalimani Meja Ndakeye (45) hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ambayo kwa kawaida inasikilizwa mahakama kuu.


Pia Hakimu Nongwa alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia washtakiwa hao dhamana sababu kiwango cha dawa wanazotuhumiwa kusafirisha imezidi kiwango ambacho mahakama hiyo inamlaka ya kutoa dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa Mashtaka. upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Novemba 13,mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.


Hivyo makala Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya

yaani makala yote Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/raia-kumi-wa-iran-na-watanzania-wawili.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Raia kumi wa Iran na watanzania wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za madawa ya kulevya"

Post a Comment