title : JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI
kiungo : JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI
JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI
NA KARIM JUMA - TANGA
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ameitaka Taasisi ya
Sayansi za Bahari wilayani Pangani Mkoani Tanga iliyopo chini ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuhakikisha wanawekeza zaidi kwenye
utafiti ili waweze kupata maendeleo makubwa.
.
Dkt Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya
Sayansi za Bahari kituo cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki
kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga.
.
Na kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah
alisema uwepo wa chuo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kitakuwa
kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Mh.DC Pangani amesema kuwa kwa sasa bado changamoto kubwa vijana na wananchi wa Pangani hawajanufaika na chuo hicho ambao wanategemea uwezekaji kwenye sekta ya uvuvi hivyo kuomba chuo hicho kuona namna ya kushirikiana na kuliona hilo na kujipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi na kuwahusisha moja kwa moja wana Pangani kupata maarifa.
.
Taarifa njema ni kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amelipokea na kulikubali na kusema wanajipanga kulianza mara moja na watajadili namna ya uendeshaji na ujenzi wa kuongeza miundombinu utaanza pia uandaaji wa mitaala ya namna hiyo kuwekwa tayari.
Hii ni faraja kubwa sana kwa wakazi wa Pangani na ni picha halisi kuwa ujio wa Chancellor Dk.Jakaya M.Kikwete umeacha alama Pangani.
Hivyo makala JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI
yaani makala yote JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/jk-atembelea-taasisi-ya-sayansi-za.html
0 Response to "JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI"
Post a Comment