MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO
kiungo : MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

soma pia


MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Mahakama kuu kanda ya Arusha imeamuru familia ya watu zaidi ya saba wenye asili ya kiasia walioondolewa kimabavu kwenye nyumba yao na kukosa mahala pa kuishi, kurejea katika Nyumba hiyo bila masharti yoyote iliyopo eneo la Sabena katikati ya Jiji la Arusha.

Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama hiyo,Thadeo Mwenempazi baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na upande wa familia hiyo kupitia Wakili wao ,Bariki Maeda na kuamuru familia hiyo kurejea katika nyumba yao wakati kesi ya msingi ikiendeleà kusikilizwa.

Jaji Mwenempazi alidai kuwa familia hiyo inapaswa kurejea katika nyumba hiyo na kuendelea na makazi wakati wakisubili maamuzi ya kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo.

Jaji katika maamuzi yake alidai kuwa mahakama hiyo imezingatia hoja zilizowakilishwa na upande wa mlalamikaji,ambaye ni familia hiyo kupitia Wakili Maeda na hivyo kuamuru kurejea katika Nyumba yao .

Familia hiyo iliondolewa kimabavu February 21 mwaka huu na kundi la watu zaidi ya 20 wakidai wanatekeleza amri ya mahakama na kusababisha usumbufu na uharibifu mkubwa wa Mali huku familia hiyo ikikosa mahala pa kuishi na kujikuta ikilala chini kwa wasamalia wema.

Akizungumza na vyombo vya habari mama wa familia hiyo,Chandni Hussein ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki na kumrejesha tena katika nyumba yake kwani taratibu zilizotumika kumtoa ndani yeye na watoto wake hazikufuatwa.

Ameongeza kuwa Nyumba hiyo iliyopo katikati ya jiji la Arusha yeye maduka ya kupanga huku familia hiyo ikiishi and a no ipo kwenye mgogoro na shemeji yake aitwaye Mortaza Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es salaam

Akizungumza huku akibubujikwa machozi mahakamani hapo mama huyo amemshukuru rais John Magufuli kwa kuendeleà kuwa mtetezi wa wanyonge ambao wamekuwa wakionewa na watu wenye kipato kikubwa cha fedha.

Kesi hiyo ya Ardhi namba 6/2019 , wakili ,Maeda ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mawakili Tanganyika Mkoa wa Arusha, aliiomba Mahakama hiyo iwarejeshe kwenye Nyumba yao hadi kesi ya msingi itakapomalizika kwa kuwa taratibu zilizotumika kuwaondoa zilikuwa na mapungufu ya kisheria .
 Pichani mama wa familia hiyo Chandni Hussein akilia kwa furaha  mara baada ya mahakama kutoa maamuzi.
 


Hivyo makala MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

yaani makala yote MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mahakama-yaamuru-familia-ya-watu-saba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO"

Post a Comment