BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI
kiungo : BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

soma pia


BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

* Yawashauri wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

BARAZA la Famasi nchini lililopo chini ya Wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto limejipanga katika kuendelea kutekeleza majukumu yao hasa kwa kuendelea kuboresha mifumo hasa ya ukaguzi, usajili pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kilichowakutanisha, Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini Elizabeth Shekalage amesema kuwa dira ya baraza hilo ni kuzidi kuwa taasisi bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kukidhi mahitaji ya jamii.

Amesema kuwa baraza hilo lina majukumu mbalimbali ikiwemo kusajili, kutambua na kutunza kumbukumbu za wanataaluma wa fani ya famasi ambao hadi sasa wataalamu wa kada hiyo waliosajiliwa imefikia 1863.

Pia amesema kuwa baraza hilo lina jukumu la kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kuwataka wananchi kutotumia dawa bila ushauri wa daktari kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Imeelezwa kuwa  baraza hilo hufuatilia malalamiko yote  yanayohusiana na usimamizi wa taaluma ya famasi yanayotolewa na wananchi na kusema kuwa wananchi wapo huru kupiga simu bure 0800110015 na malalamiko yao kutoka katika famasi na maduka ya dawa muhimu na yatafanyiwa kazi punde.

Akieleza mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Shekalage amesema kuwa baraza limefikia malengo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa moja ya taasisi ya mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa dawa (mpango wa maduka ya dawa muhimu) ambapo baadhi ya nchi zimekuja kupata ujuzi na kutekeleza mpango huo ambapo nchi za Uganda, Liberia, Zambia, Nigeria, Ghana, Burundi na Bangladesh zimejifunza namna ya utekelezaji wa mpango huo.

Pia Baraza hilo limefanikiwa katika masuala ya kusajili wafamasia, na hadi sasa baraza hilo limesajili fundi dawa sanifu 1863 na fundi dawa wasaidizi 625 huku wakijivunia uanzishwaji wa kozi ya mmoja ya utoaji wa dawa ambayi inethibitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE.)

Shekalage amesema kuwa mipango yao ya baadae kuzidi kuendelea kuboresha mifumo na wamejipanga zaidi katika masuala ya ukaguzi, usajili pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya mafunzo na maendeleo ya taaluma Grace Mallange amesema kuwa idara hiyo ambayo ina majukumu ya kusimamia mafunzo ya Famasi vyuoni ambapo inasimamia vyema katika hilo ili kuhakikisha kuwa vyuo hivyo vinazalisha wataalamu wenye tija na hiyo ni kwa kuandaa mitaala inayoongoza vyuo vyote, kuandaa na kusimamia miongozo ya kufundishia  ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha vyuo hivyo.

Mallange amesema kuwa kuwa idara hiyo pia husimamia mafunzo ya vitendo kwa wafamasia (Intership) kwa kuhakikisha wanafanya mafunzo hayo katika sehemu zinazotambuliwa  na baraza pamoja na kusimamiwa na wafamasia wanaotambuliwa na baadaye kupimwa na mitihani kabla ya kuanza kazi zao za kitaaluma.

Pia Mkuu wa Idara ya usajili na utambuzi wa viwango vya kufuzu Suma Jairo amesema kuwa wanaendelea kutumia mfumo wa kieletroniki katika usajili ili kuthibiti kughushi leseni na vibali kwa maduka ya dawa muhimu na dawa moto.

Jairo amesema kuwa mahitaji wa wafamasia bado hayatoshelezi kulingana na idadi ya wananchi waliopo huku ushauri ukitolewa kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kuweza wataalamu katika sekta hiyo.

Baraza la famasi nchini ambalo limeendelea kuratibu, kuboresha mifumo ya ukaguzi ili jamii ipate huduma bora hadi sasa imesajili wafamasia 1863, fundi dawa sanifu 2302, fundi dawa wasaidizi 652, na majengo ya kuuzia na kutunzia dawa 1683.

Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini,Bi. Elizabeth Shekalage  


Hivyo makala BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

yaani makala yote BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/baraza-la-famasi-nchini-lajizatiti.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI"

Post a Comment