Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti

Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti
kiungo : Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti

soma pia


Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti

Ndege ya Kampuni ya Coastal Aviation  iliyobeba watalii 10 imeanguka na kujeruhi watalii wawili na rubani ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Lobo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema amesema ajali hiyo imetokea jana Jumatano Oktoba 25,2017 saa tisa alasiri ilipokuwa ikitua.

Amesema taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha iliyosababisha uwanja kujaa maji.

Mwakilema amesema wakati rubani akitua ndipo ndege ilianguka na kusababisha watalii hao wawili kujeruhiwa.

“Waliojeruhiwa ni wawili na rubani ambao walipelekwa jijini Arusha na baadaye Nairobi kwa matibabu. Wengine walikuwa na maumivu kidogo ambao walipatiwa huduma na daktari wetu na baadaye wakasafirishwa kwenda Arusha,” amesema.
 
Amesema wanashukuru katika tukio hilo ndege haikuungua na kwamba, ilipokuwa ikiserereka iligonga mti na kusimama.

Mhifadhi huyo amesema mbele kulikuwa na mawe, hivyo ingeyagonga na kulipuka ingesababisha madhara makubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Mohamed Jafari hajapatikana ili kuzungumzia tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema wanaendelea kulifuatilia na kwamba, wanasubiri taarifa kutoka kwa vyombo vya uchunguzi.


Hivyo makala Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti

yaani makala yote Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/ndege-iliyobeba-watalii-yaanguka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ndege iliyobeba watalii yaanguka Serengeti"

Post a Comment