title : UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020
kiungo : UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020
UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020
Madhimisho ya wiki ya wanawake wa CCM ambapo Umoja wa Wanawake UWT wilaya ya Ubungo wameazimisha kwa kutembelea kituo cha watoto yatima Mburahati na kutoa vyakula mgeni rasmi Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT Mkoa Doroth Kilave
Picha na Heri Shaaban
Na Heri Shaaban
UMOJA wa Wanawake Wilaya ya Ubungo wamehaidi chaguzi wa mwaka 2020 chama cha Mapinduzi CCM kitashika dola katika jimbo la Ubungo na kurejesha kata zilizopotea ambazo kwa sasa zinakaliwa na wapinzani.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam Doroth Kilave wakati wa wiki ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM ambapo UWT Ubungo walimwalika Mwenyekiti wa UWT mkoa Dar es salaam mgeni rasmi
"Wanawake wa UWT ni jeshi kubwa kwa umoja wetu tutakikisha tunalinda dora chama kinashinda chaguzi zake katika jimbo la Ubungo na majimbo mengine yaliopo katika mkoa huu"alisema Kilave
Kilave alisema lengo la CCM kushika dola,amezitaka jumuiya kushirikiana na kila jumuiya kushika majukumu yake UWT ipo mstali wa mbele katika kusimamia chama.
Aidha aliwataka Wanawake wa Wiĺaya ya Ubungo kuungana katika chaguzi za Mtaa wachukue fomu wagombee wakikosa wagombe udiwani katika kata zao na Ubunge .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa UWT mkoa alisema ataka na UWT wilaya ya Kinondoni ili wagawe miradi mingine iende Ubungo kwa kuwa UWT Ubungo hawana miradi.
Katika wiki ya wanawake wa ccm Wilaya ya Ubungo UWT waliadhimisha kwa makongamano pamoja na kutembelea kambi ya watoto yatima Mburahati na kukabidhi misaada ya vyakula na kufurahi na watoto wa kambi hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa UWT wilaya ya Ubungo Sophia Kiwanga alisema wilaya ya Ubungo miongoni mwa wilaya tano zinazounda Mkoa wa Dar es saalam zimegawanyika katika tarafa mbil Magomeni na Kibamba.
Sophia alisema wilaya hiyo ina wakazi 1,031,349 kichama ina kata 14 matawi 137 idadi ya wanawake wa UWT 28,000.
Mpango mkakati kuelekea chaguzi za serikari ya mtaa UWT imeweka mkakati madhubuti kuelekea chaguzi hizo mwaka 2019.
Hivyo makala UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020
yaani makala yote UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/uwt-wilaya-ya-ubungo-yajipanga.html
0 Response to "UWT Wilaya ya Ubungo yajipanga kurejesha jimbo 2020"
Post a Comment