Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu
kiungo : Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu

soma pia


Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu

Rais John Magufuli amemteua aliyekuwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, huku aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu akiteuliwa kuwa balozi.

Dk Kashilillah ameteuliwa ikiwa ni takriban wiki tatu kupita tangu alipoondolewa katika wadhifa wa Katibu wa Bunge, nafasi iliyochukuliwa na Stephen Kigaigai.

Rais Magufuli Mei 28,2017 alitengua uteuzi wa IGP Mangu na kumteua Simon Sirro kushika wadhifa huo.

Mangu anasubiri kupangiwa kituo cha kazi pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dk Aziz Mlima.

Uteuzi wa Rais Magufuli, uliotangazwa  Alhamisi Oktoba 26,2017 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi uliwahusu pia, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na wakuu wa mikoa ambao wataapishwa  Ijumaa Oktoba 27,2017 mchana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Kijazi amesema Rais Magufuli amewateua naibu makatibu wakuu wapya saba na kuwapandisha naibu makatibu wakuu wanne kuwa makatibu wakuu kwenye baadhi ya wizara.

Pia, amewahamisha makatibu wakuu wanne na naibu katibu mkuu mmoja kwenda kwenye wizara nyingine.

Balozi Kijazi amesema katika nafasi za wakuu wa mikoa, Rais Magufuli amewateua wa mikoa sita, miongoni mwao ni aliyewahi kuwa waziri katika utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Adam Malima anayekwenda Mkoa wa Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Balozi Kijazi amesema wakuu wa mikoa walioondolewa kutokana na kustaafu ni Joel Bendera (Manyara), Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga (Geita) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Polisi, Zelothe Stephen (Rukwa).

Wakuu wa mikoa walioachwa ni wa Mtwara, Halima Dendego, Jordan Rugimbana (Dodoma) na Dk Charles Mlingwa (Mara).

Amesema Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Joackim Wagambo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Robert Gabriel amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme akiwa mkuu wa mkoa huo.

Galesius Byakanwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.



Hivyo makala Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu

yaani makala yote Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/rais-magufuli-afanya-uteuzi-wa-wakuu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Magufuli afanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, makatibu wakuu. Yumo Kashilillah, Mnyeti, Ernest Mangu"

Post a Comment