title : MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
kiungo : MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Na Mathias Canal, Singida
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka amevuliwa uongozini na Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma za kuruhusu na kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku wananchi hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.
Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya Kijiji Cha Mtavira na kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa, Mtavira na Mteva Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira Ndg Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee kuishi na kuharibu msitu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.
Mara Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza kuitishwa Mkutano wa wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya ambapo pia ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la polisi kubaini wahujumu wa msitu huo.
Mhe Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta popote alipo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu huo Jambo ambalo Ni kosa kisheria.
Usiku wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu aliongoza Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata wavamizi wa msitu wa Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo Makazi, kilimo na Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha hifadhi ya msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.
Katika Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mambo mengine pia iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa kutoa Rushwa ya fedha au Mifugo.
Hivyo makala MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
yaani makala yote MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mwenyekiti-wa-kitongoji-avuliwa-uongozi.html
0 Response to "MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU"
Post a Comment