JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA

JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA
kiungo : JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA

soma pia


JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuweka utaratibu wa kupanga miji kama sehemu ya kazi yao kuliko kukurupuka na mashinikizo ya makundi ya watu.

Naibu Waziri Mabula amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa madhimisho ya siku ya Makazi Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee.

“Halmashauri ndio zinajukumu kubwa la kupanga miji lakini cha ajabu Halmashauri nyingi zimekuwa zikipima miji kwa mashinikizo ya makundi hali inayofanya kuibuka kwa miji holela mingi katika makazi yetu” Amesema Mabula.Waziri Mabula ameongeza kuwa siku ya makazi inatukumbusha umuhimu wa kuwa na makazi bora yanayoendana na miundombinu ya huduma za kijamii.

Ameweka wazi kuwa kwa sasa Wizara yake imeweza kurasimisha nyumba zaidi ya 2000 katika eneo la Kimara na Mbezi lakini haijamaanisha kuwa zoezi hilo litaweza kuendelea nchi nzima katika maeneo ambayo yamejengwa kiholela.

Ametaja kuwa serikali itaendelea kusimamia mpango kabambe(Master Plan) wa miji yote hivyo hawatakuwa na msamaha kwa wote watakaokwenda kinyume na utaratibu wa mpango huo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Angelina Mabula akizungumza na wadau wakati wa maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , John Lupala akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Ushirika wa Nyumba (Mwenge) wakijadili jambo katika Mahadhimisho ya siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.
Wajumbe wa Ushirika wa Viguta wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri , Angelina Mabula.


Hivyo makala JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA

yaani makala yote JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/jukumu-la-kupanga-miji-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIKWEPEKI- MABULA"

Post a Comment