DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi

DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi
kiungo : DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi

soma pia


DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi

 MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi ameuomba uongozi wa Vicoba Endelevu hapa nchini kuhakikisha wanatanua mtandao wao uweze kuwafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo walimu, wafanyakazi wengine wa serikali pamoja na wafanyabiashara ndogo ndogo ili kuisaidia serikali kufanikisha adhma yake ya kuyakomboa makundi hayo kiuchumi. 


Hapi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu iliyopo Bunju wilayani humo.

“Niwaombe sana viongozi wa Vicoba mtanue zaidi mtandao wenu ili muwafikie maelfu zaidi ya wafanyabiashara ndogo ndogo, wafanyakazi mbalimbali wa serikali wakiwemo walimu na mshirikiane nao katika kuangalia namna bora zaidi ya wao kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo ili waongeze thamani ya mitaji yao,’’ alisisitiza.

Zaidi, alitoa wito kwa wakina baba wahakikishe wanahamasisha wake zao pamoja na mabinti zao waweze kushiriki katika Vicoba ili kuinua vipato vya familia zao.

“Mbali na wakina mama pia hebu tuwahamasishe zaidi wasichana ambao wamekuwa wakitumia muda na pesa zao katika urembo na kujipodoa na badala yake sasa wajenge utamaduni kujijenga kiuchumi zaidi kwa kushiriki katika vikundi hivi vya kijasiliamali pamoja na Vicoba,’’ alisema.

Awali akitoa taarifa ya hali Vicoba endelevu hapa nchini, Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola alisema mtandao huo tayari unahusisha vikundi zaidi ya laki moja vikiwa na wanachama zaidi ya milioni mbili na laki mbili huku wakiwa na akiba ya zaidi ya Tsh Trilioni moja na milioni mia mbili.

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikata utepe wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola (alieshika kipaza sauti) na Mkurugenzi wa Taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu Bi Semeni Gama (kulia kwa DC Hapi).

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikagua baadhi ya bidhaa zinazoandaliwa na wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu baada ya kizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akiongoza maandamano ya wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu kuelekea kwenye ofisi za taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam ambapo alizindua ofisi hizo mwishoni mwa wiki.



Hivyo makala DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi

yaani makala yote DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/dc-hapi-aihimiza-vicoba-kujitanua-zaidi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi"

Post a Comment