title : Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu
kiungo : Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia ya Mtandao, ambao wanatumia pikipiki yenye namba za usajili bandia MC. 759 AHW na Chassis namba PFZWFK47770 aina ya boxer.
Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Gilles Muroto aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Joseph Bakari Msinati (32) Mkazi wa Frelimo Iringa na Elisha Athman Mdemu(35)Mkazi wa Kihesa Iringa,ambao walitumia pikipiki hiyo kusafiri mikoa Mbalimbali mijini na vijijini kuiba bidhaa za dukani .
“Watuhumiwa hawa wanafika kwenye maduka na kuagiza bidhaa mbalimbali na kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa simu, Mara baada ya kulipa na mpokeaji kujiridhisha kupokea fedha hiyo wanaondoka na bidhaa. Na baada ya dakika chache wahalifu hao wanapiga simu kwenye Kampuni namba ya huduma kwa mteja na kudai kuwa warejeshewe fedha kwa kuwa wameituma kimakosa, na bidhaa kwenda kuuzwa kwa watu wengine kwa bei nafuu,” alisema Muroto.
Pia Kamanda alisema wamefanikiwa kumkamata Daudi Charles (25) Mkazi wa Mbagala akiwa na noti bandia 50 za shilingi elfu 10 ambazo zingekuwa halali thamani yake ni TSH. 500,000/=.
Katika tukio lingine Kamanda alisema wamekamata mali mbalimbali za Wizi zilizotokana na matukio ya Uvunjaji na uporaji ambazo ni Televisioni 3, Magodoro 4, Redio Subwoofer 3, Majiko ya gesi 2, Spika 3, Deck 3, mifuko ya Cement 5 pamoja na Kapeti 1.
Kamanda Muroto amewataka wananchi walioibiwa kufika polisi ili kuweza kuzitambua mali zao, Pia aliwatahadharisha Waharifu kuwa Dodoma siyo mahali Salama pa kufanyia uharifu.
Wakati huo huo Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekamata Wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao.
Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Gilles Muroto amesema kwamba ahamiaji hao walikamatwa katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Arusha kijiji cha Kuhi kata na tarafa ya Bereko Wilayani Kondoa.
Alisema Wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa na gari lenye namba za usajili T. 898 AHM na tela namba T. 422 ADD aina ya Scania mali ya Kampuni ya SANVIC LTD.
Watanzania waliokuwa wanawasafirisha Wahamiaji hawa ni Dereva Julius Jackson Kitoma(57) Mnyaturu na mkazi wa Ngarenaro Arusha, Abedi Raphael Nyomolelo (20) Utingo wa gari hilo na Mkazi wa Sakina Arusha.
Wengine ni Ramadhani Salumu Mawazo (39)Mzaramo pia mkulima na mkazi wa Mbagala Dar es Salaam pamoja na Juma Ramadhani Husei (46) Mzigua, mkulima na mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam, aliwataja Muroto. Aidha alisema kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu ya kuwafungia Wahamiaji hao kwenye Contena la Mizigo, wakiwachanganya na bidhaa walizokuwa wakizisafirisha ambazo ni maboksi yenye Vizibo vya Soda na bia kutoka Namanga- Arusha kuelekea Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma ACP Gilles Muroto akiwa na sehemu ya wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao.
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma ACP Gilles Muroto akiwa na mmoja wa watuhumiwa wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia ya Mtandao.
Hivyo makala Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu
yaani makala yote Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/jeshi-la-polisi-mkoani-dodoma-wanasa.html
0 Response to "Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu"
Post a Comment