title : WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO
kiungo : WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO
WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.
Hivyo makala WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO
yaani makala yote WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/waziri-mkuu-majaliwa-atembelea-mradi-wa.html
0 Response to "WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO"
Post a Comment