WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI
kiungo : WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

soma pia


WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo nunua mazao ya wakulima nchini.

Wakati NFRA imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.Alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haitalifumbia macho kamwe.

Pamoja na mambo mengine waziri Hasunga ameupongeza Uongozi wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo nane ya kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akisalimiana na Mwenyeji wake ambaye ni Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Ndg Nicodemus Massao wakati alipowasili kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.



Hivyo makala WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

yaani makala yote WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/waziri-wa-kilimo-azitaka-nfra-na-bodi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI"

Post a Comment