title : WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA
kiungo : WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA
WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA
Na John Nditi, Ulanga.
KAMPUNI ya TanzGraphite imesema itawajengea nyumba zenye hadhi ya juu kaya za kijiji cha Epanko, wilayani Ulanga , mkoani Morogoro zinazohama kwa kupisha mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya Kinywe (Graphite) na itahakikisha kuwa, maisha ya watu wanaohama yanabaki kama ilivyokuwa awali ikiwa na kuboreshwa zaidi.
Meneja Mahusiano wa TanzGraphite, Bernard Mihayo , alisema hayo kwenye taarifa ya Kampuni hiyo katika kikao cha tisa cha kikosi kazi kilichokutana Septemba 14, mwaka huu mjini Mahenge , wilayani humo.
Kikao hicho kilichokuwa ni cha kujadili na kupokea mrejesho wa vikao vya wananchi kuhusu mpango wa uhamishaji makazi (RAP) kupisha mradi wa madini ya kinywe wa Epanko kilihudhuriwa na wajumbe wa vitongoji vya Kazimoto, Epanko A, Itatira , Mbera, Epanko B na Luli .
Wawakilishi wengine ni kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Ofisi ya madini mkoa , Ofisi ya wilaya ya Ulanga , halmashauri na wadau wengine wa mradi huo.
Madini ya Graphite ‘Kinywe’ kwa sasa yanahitajika kwa wingi duniani kutokana na matumizi ya kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo betri za simu , kompyuta mpakato ‘laptop’ na penseli .
Kiongozi wa wa kimila wa kabila la Wapogoro wa kijiji cha Epanko , wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro (Mbuyi ), Redemta Masura ( wapili kushoto) akiwa na viongozi wa Kijiji hicho wakipitia taarifa ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko , wakati wa kikao cha tisa cha Kikosi Kazi iliyowashirikiasha wajumbe wa kutoka vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali na kijamii kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Baadhi ya viongozi wa serikali wa wilaya ya Ulanga na mkoa wa Morogoro wakiungana na vitongoji vya kijiji cha Epanko wakiwemo na wakimila na kijamii kupitia taarifa ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko katika kikao cha tisa cha Kikosi Kazi cha mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya Kikosi kazi kutoka serikali za vitongoji vya kijiji cha Epanko wakiwemo wa kimila na kijamii wilayani Ulanga wakijumuika na wa ngazi ya wilaya hiyo na mkoa wa Morogoro kupitia kwa pamoja taarifa ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Lucas Mwaisaka (kulia) akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Epanko, Kata ya Nawenge, wilayani Uanga, Eliza Liwemba, ( kushoto) Mpango wa Uhamishaji Makazi (RAP) wa Mradi wa Madini wa Epanko wakati wa kikao cha tisa cha Kikosi Kazi cha mpango huo kilichowashirikisha wajumbe wa kutoka vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali ya wilaya na mkoa ambacho kilifanyika hivi karibuni mjini Mahenge. ( Picha na John Nditi).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA
yaani makala yote WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/wanaopisha-mradi-mkubwa-wa-uchimbaji.html
0 Response to "WANAOPISHA MRADI MKUBWA WA UCHIMBAJI MADINI YA ‘KINYWE’ KIJIJI CHA EPANKO KUFAIDIKA KWA KUJENGEWA NYUMBA ZA KISASA ENEO MBADALA"
Post a Comment