title : SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
kiungo : SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 11 ili kukabiliana na utapiamlo na amemtaka kila mdau wa lishe aonyeshe bayana mchango wake katika kukabiliana na utapiamlo nchini.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Septemba 6, 2017) wakati akifungua mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa lishe wa kutathmini afua za lishe nchini kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Pia alizindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 (Joint Multisectoral Nutrition Review).
“Viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali wabaini kiwango cha utapiamlo katika maeneo yao, waonyeshe mbinu za kukabiliana na hali hiyo, wafanye tathmini ya ufanisi na watoe taarifa za ufanisi,” amesema.
Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote, wahakikishe shilingi 1,000 ambazo Halmashauri zilielekezwa kutenga kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vyao vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano, zinatolewa na kutumika kama ilivyopangwa.
“Tulikubaliana kila Halmashauri lazima ikusanye makusanyo ya ndani kwa asilimia zaidi ya 80. Nilisema kiwango cha chini kisipungue asilimia 80. Na kupitia makusanyo hayo, ndipo tunapata fedha za kutenga kwa masula kama haya,” alisisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu, kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hivyo makala SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO
yaani makala yote SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/serikali-yatenga-shbilioni-11-kukabili.html
0 Response to "SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 11 KUKABILI UTAPIAMLO"
Post a Comment