WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI
kiungo : WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI

soma pia


WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kukumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo mapema leo Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu. Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.

"Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee" alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.

Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu. "Kwanza nikupe pole kwa ajari. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana" alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music."Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja" alisema Mxcater.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu. Kulia kwa Waziri ni Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa 'Mxcater'.NA  ANDREW CHALE,DAR.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu.



Hivyo makala WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI

yaani makala yote WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-dktkigwangalla-apokea-gold-moi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA GOLD MOI"

Post a Comment