title : MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
kiungo : MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo: Makampuni ya Kimataifa na Kitaifa yanayoendesha shughuli za kibiashara hapa nchi makubwa kwa madogo yanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa kuheshimu haki za binadamu na kuwajibika pale yanapokiuka haki hizo.
Hayo yameelezwa leo mjini Bagamoayo na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Obadia Kameya, wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji kwa Maafisa wa Serikali kuhusu Biashara na Haki za Binadamu. Bw. Kameya amesema, Makampuni ambayo yatabainika kukiuka haki za binadamu katika uendeshaji wa shughuli zao, yanapashwa kuchukuliwa hatua na kwamba mwenye wajibu huo ni Serikali ambayo ndiyo inayobeba dhamana kwa mujibu wa Katiba ya kuhakikisha kwamba haki za wananchi wake ndani ya mipaka yake zinalindwa, kusimamiwa na kutetewa.
Ni kwa sababu hiyo, Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Maafisa wa Serikali ambao kwa namna moja ama nyingine wanahusika na masuala ya Biashara na Haki za Binadamu wanapashwa kuwa na uelewa mkubwa kuhusu Kanuni na Miongozo inayohusu Haki za Binadamu na Biashara.
Akasema , suala la Biashara na Haki za Binadamu limekuwa ajenda ya ulimwengu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuhusishwa kwake na haki za binadamu na ni katika muktadha huo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mshauri wa Serikali kuhusu mauala ya Sheria, imeamua kwa Kushirikiana na Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika (OHCHR-EARO) kuandaa mafunzo ya kuwajenga uwezo Maafisa wa Serikali.
Bw. Kameya akasisitiza zaidi kwa kueleza kwamba, ni muhimu sana kwa Maafisa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Maafisa kutoka Wizara nyingine za Serikali na Taasisi kuwa na utambuzi wa masuala ya Biashara na Haki za Binadamu ambayo yaathari kwenye sera, sheria, mikataba na makubaliano ya kimataifa na katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali na hasa katika kipindi hiki ambacho nchi imejielekeza kuwa nchi ya Viwanda.
Naye Mwakilishi wa OHCHR EARO Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor amesisitiza kwamba ingawa Maaofisa wa Serikali wanaowajibu wa msingi kabisa wakuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu na kuhakikisha kwamba Makapuni ya Kibashara yatekeleza na kuwajibika katika kuhakikisha kwamba hayakiuki misingi na kanuni za haki za binadamu na kwamba yajifanyia tathimini na kutoa taarifa kama inavyotakiwa.
Wawezeshwaji wa Mafunzo hayo wakiongozwa na Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor ambaye ni Mwakilishi wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika ( OHCHR-EARO) walifundisha kuhusu Mfumo wa Umoja wa Mataifa ulioridhiwa mwaka 2008 unaojulikana kama Zuia, Heshimu na Fidia kuhusu Biashara na Haki za Binadamu.
Mfumo huu wa Umoja wa Mataifa una Misingi Mikuu Mitatu. Wa Kwanza ni kuhusu wajibu wa serikali kwa kuzingatia sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ya kumlida kila mtu ndani ya mipaka yake na katika eneo la mamlaka yake kwa kuweka sheria madhubuti , kanuni , sera ikiwa ni pamoja na kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Makampuni ya Kibiashara. Msingi wa Pili wa mfumo huu unazitaka Kampuni za Biashara kuwajibika katika kuheshimu haki za binadamu mahali popote zinakoendesha shughuli zao bila ya kujali ukubwa au udogo wa biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kutambua madhara yatokanayo na shughuli zao na kuchukua hatua za kuzuia madhara hayo.
Msingi wa Tatu ni utoaji wa fidia kutokana na athari za ukiukwaji wa haki za binadamu unaotokana na shughuli za kibiashara zinazofanywa makampuni hayo. Baadhi ya athari hizo zinatajwa kuwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira, ajali kazini, malipo au ujira duni, uhamishwaji wa kutumia nguvu na usiozingatia sheria.
Washiriki wa Mafunzo hayo wametoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Biashara na Viwanda, Tume ya Kurekebisha Sheria , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kituo cha Uwekezaji, Nishani na Madini, na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Washiriki wa Mafunzo ya Uwezeshaji kuhusu Biashara na Haki za Binadamu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo. mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika mjini Bagamoyo na yameandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika (OHCHR EARO). Mafunzo hayo yalifunguliwa na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Obadia Kameya aliyeketi katikati kushoto kwake ni Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor na kulia ni Bi. Cecilia S. Shelly- Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Pwani.
Hivyo makala MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
yaani makala yote MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/makampuni-ya-biashara-yatakiwa.html
0 Response to "MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU"
Post a Comment