Baraza la Ardhi Mkuranga

Baraza la Ardhi Mkuranga - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Baraza la Ardhi Mkuranga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Baraza la Ardhi Mkuranga
kiungo : Baraza la Ardhi Mkuranga

soma pia


Baraza la Ardhi Mkuranga



 Image result for PICHA ZA NEMBO YA MAHAKAMA TANZANIA
Na Hussein Ndubikile, 
Mwambawahabari, Pwani
Mwenyekiti wa Ba Baraza  la Ardhi na Nyumba la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Rehema  Mwakibuja amewaondoa wadaiwa wawili akiwemo Omari Issa na Bakari Saguti katika kesi ya msingi msingi ya mgogoro wa ardhi kati ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), Adelardus Kilangi ambaye ni mdai dhidi ya wadaiwa zaidi ya 70 ambao ni wananchi wa Kijiji cha Vicheji kilichopo wilayani humo licha ya wadaiwa hao kudai hawawezi kutoa maelezo sababu kuwa Wakili wao hayupo.

Hatua hiyo imekuja baada  ya wadaiwa hao kutakaa kutoa maelezo kwa kuwa wakili wao alipata ajali na taarifa walishatoa huku kila mmoja akisisitiza tayari wameshafanya mazungumzo ya awall na wakili mpya hivyo tararibu zitakapokamilika wataaendelea na kesi.

Mwenyekiti  wa baraza hilo alituipilia mbali ombi hilo kwa kueleza kuwa kesi imeshaletwa mezani hivyo lazima iendelele kusikilizwa na kwamba waliokataa kuzungumza amewafuta majina yao.

Kwa upande wa mdaiwa, Juma mauge alipotakiwa kutoa maelezo alidai hawezi kuongea kwa ufasaha kwa ametoka kwenye msiba wa mama yake mzazi, hivyo mwenyekiti alimkubalia na kumtaka aende akajiandae atapokuja kesi iendelee kusikilizwa.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliwaambia wadaiwa waliofika katika baraza hilo hakuna sheria inayoelezea wadaiwa kutoa maelezo kwa mtiririko wa watu waliowapanga hivyo baraza hilo lina uwezo wa kumchagua yeyote kati  yao na si vinginevyo.

Mgogoro katika kesi namba 55 ya mwaka 2016 unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary 40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55) ,Sada Abdallah(72)  na ambao kwa pamoja wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.

Washitakiwa hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei 9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya AG  Kilangi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.


Hivyo makala Baraza la Ardhi Mkuranga

yaani makala yote Baraza la Ardhi Mkuranga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Baraza la Ardhi Mkuranga mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/baraza-la-ardhi-mkuranga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Baraza la Ardhi Mkuranga"

Post a Comment