title : TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.
kiungo : TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.
TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.
Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii.
Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.
Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.
Hivyo makala TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020.
yaani makala yote TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/taasisi-ya-thps-yazindua-mpango-mkakati.html
0 Response to "TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020."
Post a Comment