title : MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA
kiungo : MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA
MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, amewataka askari wa uhamiaji nchini kuhakikisha wanataifisha magari na vyombo vya usafiri wanavyokutwa navyo wahamiaji haramu, wakati wanapokamatwa. Aidha amewaagiza askari hao kuwakamata watu wanaowalipia faini wahamiaji haramu na kuwafungulia mashitaka.
Mwigulu aliyasema hayo, wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi mpya ya uhamiaji ya mkoa wa Pwani ambazo zote zipo wilayani Kibaha. Alisema magari na vyombo vinavyosafirishia wahamiaji haramu ikiwemo boti vitaifishwe na kutumika katika kazi za ujenzi wa taifa.
"Haiwezekani mtu aingie nchini kwa makusudi bila kibali halafu inapotakiwa kulipa faini kutokana na kosa hilo atokee mtu kuwalipia faini kwa haraka jambo linalosababisha vitendo hivyo kuenea kwa kasi” alisema Mwigulu.
Mwigulu alieleza kwamba, ni lazima iangaliwe, jamii inapaswa kujiepusha na kushirikiana na kundi hilo ili kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji haramu nchini. Waziri huyo alisema, iangaliwe njia za kudhibiti wahamiaji hao pale inapotokea kukamatwa ama kushtakiwa na kuhukumiwa pasipo kuwalinda kwa kuwalipia faini.
"Mkiwakamata pia na magari myataifishe siku hiyo hiyo na kuyapeleka magereza ili yakabebe mawe, na hata mkiwakamata kwenye boti taifisheni hizo boti hakuna kuweka viporo"alisema Mwigulu.
Awali akitembelea ofisi mpya katika jengo la vitambulisho vya taifa (NIDA), Mwigulu aliwaagiza watendaji wa ofisi hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuunganisha utambulisho wa jumla kwa wananchi.
"Wananchi wanatakiwa wawe na utambulisho wa aina moja pekee unaojumuisha taarifa zao zote" alisisitiza Mwigulu.
Nae afisa Uhamiaji Mkoani Pwani, Plasida Mazengo alisema ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitendea kazi hali inayosababisha kufanyakazi kwenye mazingira magumu. Alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kusaidia kutatua changamoto hizo ili waweze kufanya kazi zao kifanisi zaidi kwa maslahi ya watanzania.
Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9, na utakapokamilika utawarahisishia wananchi kupata huduma kirahisi na jengo litaanza kazi rasmi mwishoni mwa mwezi huu .
Hivyo makala MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA
yaani makala yote MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/magari-boti-wanavyokutwa-navyo.html
0 Response to "MAGARI, BOTI WANAVYOKUTWA NAVYO WAHAMIAJI HARAMU VITAIFISHWE - NCHEMBA"
Post a Comment