title : Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini
kiungo : Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini
Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameyashauri mabenki ikiwemo NMB kubuni bidhaa zitakazowanufaisha Watanzania maskini ili kuondoa dhana inayowabaguzi ya kuwa "‘maskini sio rafiki wa taasisi za kifedha". Mtaturu ametoa wito huo juzi wakati akifungua rasmi Tawi la Benki ya NMB Ikungi.
Alisema kuendelea kuamini kwamba maskini sio rafiki wa mabenki, kundi hilo la Watanzania litaendelea kudidimia ndani ya lindi la umaskini. “Kaeni muangalie kundi hili la watu maskini litanufaikaje na huduma zinazotolewa na mabenki ikiwemo ninyi NMB.
Kundi hili la Watanzania maskini ili liweze kujikomboa kiuchumi, basi mabenki badala ya kutoa mikopo ya fedha taslimu, toeni mikopo ya mizinga ya nyuki, mabwawa ya kufungia samaki au kuku kwa ajili ya kufunga kibiashara”, alishauri Mtaturu.
Akisisitiza,mkuu huyo wa wilaya, alisema ili Mtanzania akiwemo maskini aweze kupata maendekeo ya kweli ni lazima ajiongeze kwa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha. “NMB ninyi mnakwenda vizuri na mnakwenda na wakati.
Mmeendelea kubuni bidhaa/huduma mbalimbali ambazo zimepelekea kuvutia Watanzania zaidi ya milioni mbili kufungua akaunti kwenye matawi yenu nchini kote”, alisema na kuongeza; “Sasa mmebuni akaunti ya FANIKIWA, ambayo inawalenga wajasiriamali wadogo wakiwemo baba/mama lishe na wauza chips. Hongereni sana”.
Meneja wa NMB kanda ya Kati, Straton Chilongola (wa tano kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni tano vilivyotolewa na NMB.
Mtaturu alisema sasa umefika wakati wa kuliangalia upya kundi la Watanzania maskini,ili na lenyewe liweze kushiriki kikamilifu kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati. Aidha, Mtaturu ametumia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa wilaya ya Ikungi wahakikishe wananufaika kikamilifu na huduma mbalimbali zinazotolewa na tawi la NMB Ikungi.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini
yaani makala yote Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/benki-zashauriwa-kubuni-bidhaa-zitakazo.html
0 Response to "Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini"
Post a Comment