title : PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE
kiungo : PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE
PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE
Shirika la ndege la Kitanzania Precision Air limezindua kwa mafanikio safari zake za kwenda Entebbe. Ndege ya uzinduzi wa safari hizo iliondoka Jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:10 asubuhi leo kuelekea Entebbe na kuwasili Entebbe majira ya saa 4:50 Asubuhi na kupokewa kwa salamu maalumu ya kumwagiwa maji na magari ya zima moto, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa zama mpya za huduma za Precision Air kati ya Tanzania na Uganda.
Akizungumzia kuanza rasmi kwa safari hizo Meneja Uratibu na Mahusiano Bw. Hillary Mremi amesema kuwa, kupitia safari za Precision Air Tanzania na Uganda wamehakikishiwa usafiri wa uhakika.
“Tutakuwa tukifanya safari mara tatu kwa wiki, kila siku ya Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi na baadaye kuongeza safari kulingana mahitaji ya soko.” Amekaririwa Bw. Mremi Precision Air iliahirisha safari za Entebbe mnamo mwaka 2013 kupisha maboresho ya mtandao wa wa safari zake katika kuhakikisha inazingatia tija katika shughuli zake.
Precision Air ndilo Shirika pekee la ndege linalotambuliwa na IATA ambalo linafanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Uganda. Inatarajiwa safari hizi za Precision zitaimarisha mahusuano ya kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda, hasa ikizingatiwa kuwepo kwa miradi mbali mbali ya pamoja kama ule wa bomba la mafuta litakalo anzia nchini Uganda hadi Tanzania.Ni miradi kama hiyo inayotarijiwa kunufaika na safari za Precision Air kwa kufanikisha miradi hiyo kwa wakati.
Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11. Iktokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar na Nairobi.
Hivyo makala PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE
yaani makala yote PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/precision-air-yaanza-safari-za-entebbe.html
0 Response to "PRECISION AIR YAANZA SAFARI ZA ENTEBBE"
Post a Comment