Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto

Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto
kiungo : Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto

soma pia


Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto


Mafia. Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi tawi la Mshonzini iliyopo wilayani Mafia mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho.
Akithibitisha tukio hilo, Katibu wa CCM wilayani Mafia Mohammed Dhikiri amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 13.
Dhikiri amesema moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo pamoja na samani za ndani.
Amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama.
Amesema bado halijafahamika ni nani aliyehusika na tukio hilo na kueleza kuwa wameliachia Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi zaidi dhidi ya tukio hilo.
Awali akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau alisema vipo viashiria vinavyoonyesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo.
Dau amesema mtu huyo baada ya kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zilivyoonyesha.
Amesema hilo ni tukio la kwanza kutokea wilayani humo kwa kuwa hadi linatokea hapakuwa na viashiria vyovyote vile vya kutokuwepo kwa Amani kati ya wanachama au viongozi.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga simu yake iliita bila kupokelewa.
chanzo, mwananchi


Hivyo makala Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto

yaani makala yote Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/ofisi-ya-ccm-mafia-yachomwa-moto.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ofisi ya CCM Mafia yachomwa moto"

Post a Comment