MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

soma pia


MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini wanapata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.

“Ningependa kusema kwamba Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani kupanua ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta ya simu ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja wa Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza Makamu wa Rais.

Ameleeza kuwa kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo huwasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu,afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).




Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM"

Post a Comment