Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza

Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza
kiungo : Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza

soma pia


Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza

Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya nchi ipasavyo.

Williams imeelezwa ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo, akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.

Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.





Hivyo makala Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza

yaani makala yote Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/majadiliano-kati-ya-tanzania-na-kampuni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza"

Post a Comment