AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA

AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA
kiungo : AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA

soma pia


AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA

Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania imetoa msaada wa magari mawili aina ya Nissan Patrol kwa halmashauri za wilaya za Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri hizo.

Magari hayo yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yana thamani ya shilingi milioni 186 yamenunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).

Hafla fupi ya Makabidhiano ya magari, imefanyika leo Jumatatu Novemba 5,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Mkuu huyo wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema msaada huo wa magari ni kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya hususani za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma.

Dkt. Mwakyusa alisema, AGPAHI imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na halmashauri katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Magari yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yenye thamani ya shilingi milioni 186 yaliyonunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa,Crispin Luanda na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella (wa tatu kulia) wakioneshana magari yaliyotolewa na AGPAHI.
Muonekano wa magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Buchosa.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.



Hivyo makala AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA

yaani makala yote AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/agpahi-yatoa-msaada-wa-magari-kuboresha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MWANZA"

Post a Comment